Gegen-Pressing ilivyotambulisha mbinu za Klopp
Sisti Herman
February 26, 2024
Share :
Utangulizi
Klabu ya Liverpool jana imetwaa ubingwa wa kombe la ligi nchini Uingereza maarufu kama EFL Cup au Carabao Cup baada ya kuwanyuka Chelsea 1-0 kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Hii ni sehemu ya tathmini yangu kumhusu kocha Jurgen Klopp baada ya jana kuiongoza Liverpool kutwaa taji hilo akielekea mwishoni mwa msimu baada ya kuaga wiki kadhaa zilizopita na kuthibitisha kuwa utakuwa msimu wake wa mwisho na majogoo wa London baada ya miaka 9 huku akitwaa mataji makubwa kama;
• UEFA Champions league 1
• UEFA Super Cup 1
• FIFA Club World Cup 1
• Premier league 1
• FA Cup 1
• EFL Cup 2
• Community Shield 1
Fundi wa Gegen-Pressing
Klopp anaaminika kuwa ndiye kocha aliyefanikiwa zaidi na staili ya uzuiaji ya Gegen-pressing ambayo imekuwa maarufu zaidi duniani baada ya kutwaa nayo mataji makubwa kuliko makocha wengine waliowahi kuitumia.
Utambulisho na asili ya GEGEN-PRESSING
Baada ya kuwasili Uingereza mwaka 2015 kocha huyo alitambulisha staili ya uzuiaji maarufu zaidi nchini Ujerumani inayojulikana Gegen-pressing au German Pressing ambayo iliasisiwa tangu Karne iliyopita na kocha wa zamani wa Urusi Victor Maalov na kuendelezwa na kocha Muitaliano Arrigo Sacchi na kocha na mkurugenzi wa michezo Ralf Ragnic
Gegen-pressing ni staili ya uzuiaji ambayo timu inayozuia huzuia kwa shinikizo kubwa kwa timu inayoshambulia na kuwalazimisha kupoteza mpira kwenye eneo mpira ulipo hasa kwenye theluthi ya ujenzi wa mashambulizi ya timu inayoshambulia "high press" au popote mpira utakapopotea "Counter Pressing"
Klopp alivyofanikiwa nayo
Klopp alitambulishwa na mbinu hizi bora za uzuiaji akiwa na Liverpool baada ya kujiunga nayo mwaka 2015 na kuanza kuipandikiza mbinu hiyo.
Mfumo: 4-3-3
Klopp alitumia mfumo wa 4-3-3 ambao kwenye ubora wao alikuwa na wachezaji kama;
- Allison Becker (GK)
- Andrew Robertson (LB)
- Trent Alexander-Arnold (RB)
- Virjil Van Dijk (CB)
- Joel Matip (CB)
- Fabinho (DM)
- Jordan Henderson (RCM)
- Georginio Wijnaldum (LCM)
- Mohamed Salah (RF)
- Sadio Mane (LF)
- Roberto Firminho (CF)
Staili: Gegen-pressing
Wakizuia Liverpool walizuia kwa pamoja kuanzia kwenye theluthi ya Kwanza ya ujenzi wa mashambulizi ya Wapinzani (Build up phase) kwa shinikizo kubwa wakiwa na nia ya;
• Kupora mpira na kujibu shambulizi kwenye maeneo ya juu ya uwanja
• Kulazimisha wapinzani wapige mipira mirefu ambayo ni ya kushindania juu
Liverpool walifanya Pressing kwa kuzuia kuanzia juu kwa malengo hayo mawili Wakiamini kuwa ni rahisi zaidi kufunga Kwa staili hiyo kuliko njia ya kujenga mashambulizi kuanzia golini kwao huku wapinzani wakiwa wamejipanga kuwazuia, Badala yake waliona ni rahisi kupora mipira kwa kuwashinikiza kufanya makosa na kuwashambulia kabla hawajajipanga kuwazuia
Liverpool walichanganya namna mbili za uzuiaji kwa wakati mmoja, Kuzuia nafasi (Zonal marking) na kuzuia watu (Man marking), mfano wakizuia
• Mstari wa Kwanza wa uzuiaji wa watu watatu ukianza kuzuia kuanzia kwenye theluthi ya ujenzi wa mashambulizi ya Wapinzani (Build up phase);
- Mane na Salah huzuia njia za pasi kutoka kwa mabeki wa kati wa timu pinzani (Opposition CB) kwenda kwa mabeki wa pembeni (Opposition FB)
- Firminho huzuia njia za pasi kutoka kwa kipa na mabeki wa timu pinzani kwenda kwa kiungo/viungo wa kati
• Mstari unaofuata huwa na watu wawili, Wijnaldum na Henderson ambao huzuia mabeki wa timu pinzani na viungo viungo wasiendeleze shambulizi
•Lengo la Kwanza la Mistari hii miwili huwa ni kupokonya mpira na kujibu shambulizi maeneo ya mbele ya uwanja ili kushambulia nafasi kabla wapinzani hawajarejea kwenye miundo yao ya uzuiaji (Positive Transitions) au kulazimisha
• Lengo la pili la mistari hiyo ya mbele kushinikiza wakiwa pamoja na kwa presha kubwa ni kulazimisha wapinzani wapige mipira mirefu mbele ili iwe ya kugombania 50/50 huku wao wakijipanga kuwa wa Kwanza kushinda mipira ya juu (Aerial duels) na mipira inayodondoka (Second balls)
• Kazi ya Mistari mwili ya nyuma yenye watu watano inayojumuisha mabeki wanne (VVD na Matip Kati, Trent na Robertson pembeni) na Kiungo mmoja mzuiaji (Fabinho) ni kuhakikisha mstari wa mbele ukienda wao hushinda mipira yote ya kugombania inayovuka Pressing Structure Yao iwe ya juu au chini
• Pia Mbinu hizi zilimtegemea Allison Becker kuwa kama msafishaji nyuma ya mabeki (Sweeper keeper) ambapo alikua anasogea hadi nje ya Box lake kusafisha hatari zozote zinazoangukia nyuma ya mabeki wake.
Utawala Wakishambulia
Ukiachana na staili ya kushambulia kwa kujibu Liverpool kwenye mbinu zao pia walikuwa na Mbinu za kuwatawala mchezo kwa kuhakikisha nyakati zote unakuwa kwenye umiliki wao
Mfumo: 4-3-3 to 4-4-2 diamond (4-1-2-1-2)
Liverpool huutumia muundo wa 4-1-2-1-2 ambao hunyumbulika kuwa kwenye miundo tofauti Kama;
Build Up; Hujenga shambulizi na muundo wa 3-3-2-1-2 wakimjuisha kipa na kutengeneza muundo wa 3+3 kwenye mistari miwili ya nyuma ambapo kwenye ujenzi wa mashambulizi Allison Becker huwa Katikati ya mabeki wawili wa kati Matip na VVD dhidi ya mstari wa mbele wa timu inayozuia
Progressions; Mstari huu husaidiwa na watatu wanaofuata kwaajili ya kuendeleza shambulizi, Fabinho kwa njia Katikati kwa kupokea pasi nyuma ya mstari wa washambuliaji wa timu pinzani au njia za pembeni kwa Trent na Robertson.
Penetration & Creation; akiwa kwenye nusu ya wapinzani Liverpool huwa kwenye muundo wa 2-3-5, ambapo hutegemea pembetatu za wachezaji wa pembeni kupenya na Kutengeneza nafasi;
• Kulia hutegemea Combination ya Trent na Salah kwenye mapana ya uwanja huku wakiunganishwa na Henderson anayecheza nafasi ya Kati upande huo
• Kulia hutegemea Combination ya Roberson na Mane kwenye mapana ya uwanja huku wakiunganishwa na Wijnaldum anayecheza nafasi ya Kati upande huo
Wachezaji hawa wa pembeni walibadilishana sana nafasi, hasa Viungo na mabeki ili kusaidia kufunguka kuwachanganya wazuiaji na kutanua Kuta za uzuiaji hasa wanapofika ambapo mara nyingi;
• Trent na Robertson hushambulia mapana ya uwanja kutanua kuta za wazuiaji pembeni (mara kadhaa Trent hubadilishana na Henderson)
• Mane na Salah hushambulia mianya kati ya CB na FB wa wapinzani baada ya kuta kutanuliwa
• Hawa wote huunganishwa na Henderson na Wijnaldum
Pia Firminho hushiriki Matendo ya timu kupenya na nafasi Kutengenezwa, mara nyingi huenda kuongeza idadi mpira ulipo na kusaidia timu kupenya kuta za wazuiaji, mfano;
• Liverpool ikiwa kwenye presha, yeye hushuka katikati ya mistari kusaidia kuongeza idadi eneo hilo
• Mpira ukiwa pembeni huenda kuongeza idadi kwenye zile Wide triangles na Kutengeneza Wide Overloads ambapo situation za 4v3 hutengenezwa na timu kuvuka kwa faida ya idadi (numerical Superiority)
Firminho hufanya mikimbio ya kurudi Katikati ya mistari na kusaidia majukumu ya kupenya kwani anaporudi chini huondoka na mabeki wanaomfuata mfuata na kuacha mianya kwa Mane na Salah
Hao wote wa nyuma hulindwa na Fabinho ambaye nyakati zote husimama mbele ya mabeki wa kati kulinda Counter Attacks zisiwaathiri Pindi wachezaji wake wa mbele wabapopoteza mpira
Kutumia Ubunifu na Idea za soka la kisasa
Klopp pia hakuachwa na dunia, kila mbinu za mchezo zilipofanyiwa maboresho kulingana na mapungufu yanayovumbuliwa kila kukicha yeye pia alienda na kasi hiyo, hizi ni baadhi ya idea mpya za soka la kisasa alizozitumia kuboresha mbinu zake;
Modern Goalkeeper
Baada ya tafiti nyingi kugundua kuwa mipira mingi mpirefu inayoanzia nyuma inayopigwa kwa washambuliaji na inakuwa ya kugombania na mingi wanashinda wapinzani, wataalamu walikuja na suluhisho la kujenga mashambulizi kwa pasi fupi kuanzia nyuma kwa kipa kuanzia kwenye theluthi ya kwanza, kisha wakazaa faida kubwa kama;
- Kuwavuta wapinzania na kuongeza kina cha uzuiaji kinachotengenezeka hutengeneza mianya katikati ya mistari ya uzuiaji ambayo husaidia timu kupenya na kufika kwa wapinzani
Lakini kipa huyo pia alitumika kama msafishaji wa mipira yote ya hatari ambayo huelekezwa nyuma ya mstari wake wa Ulinzi
Inverted Full Back
Baada ya tafiti nyingi kugundua kuwa timu zinazomiliki mpira sana hasa kwenye nusu ya wapinzani hufanyiwa sana mashambulizi ya kujibu pindi wanapopokonywa mpira ambayo huwaathiri kwasababu ya muundo ambao zinakuwa zimeuacha kwenye mistari miwili ya nyuma pindi wanapokuwa kwenye theluthi za mwisho kuelekea kwa wapinzani kuwa na uchache na nafasi kubwa baada ya kutanua, wataalamu wakavumbua namna mbalimbali za kuepuka madhara hayo kwa kuweka muundo mzuri ambao huweka sawa uwiano wa idadi ya watu na nafasi kwenye mistari hiyo ambayo huweza kupunguza madhara hayo (Rest Defence).
Moja ya utatuzi ni mikimbio ya mabeki wa pembeni kuingia ndani huku wakiendelea kuchangia timu kupenya kuta za wazuiaji huku wakiruhusu wachezaji wa mbele kutanua uwanja, kwenye jukumu hili Klopp aliona Trent anafaa kucheza kama beki wa pembeni ambaye timu yake inamiliki mpira huongeza idadi eneo la kiungo huku winga wake akitanua pembeni.
Kwakufanya hivyo Pep aliboresha mistari yake ya ulinzi kwani timu yake ikipigwa Counter Attack kabla ya mabeki wa kati kufikiwa kuna layer yenye watu wawili, kiungo mzuiaji na Trent ndipo wafike lakini pia imeongeza umiliki wa mpira kwani idadi huruhusu kuwa na mpira nyakati nyingi
False 9
Kuna nyakati timu pinzani huwa zikicheza na timu kubwa huenda na nidhamu kubwa sana ya uzuiaji ikiwa na pamoja kujaza idadi kubwa ya viungo ili kuzuia hatua muhimu za build up kama progression, penetration na creation, wataalamu wa mbinu wakaja na mbinu ya kumtumia mshambuliaji wa kati ambaye huweza kushuka hadi katikati ya mistari kucheza kama kiungo kusaidia hatua hizo muhimu kuanzia timu kuendeleza mashambuliz, kupenya kuta za wazuaji na kutengeneza nafasi.
Mshambuliaji huyo akaitwa mshambuliaji kivuli, False 9, ambapo kwa Klopp alimtumia Firminho, na kuunyumbulisha mfumo wake pendwa wa 4-3-3 kuwa 4-4-2 ambapo Firminho timu ikiwa na mpira kwenye theluthi za nyuma hushuka hadi katikati ya mistari mbele ya Henderson na Wijnaldu kuwa kama namba 10 na kuwaacha Salah na Mane mbele, lakini ikizuia huwa mbele.