GEITA: Mwanamke adai kazaa ndege!
Eric Buyanza
March 12, 2024
Share :
Semeni Msumeno, mkazi wa mtaa wa Kigoma Road katika Halmashauri ya Mji wa Geita amedai kuwa amejifungua (amezaa) kitu kinachosadikika kuwa ni ndege, jambo ambalo limeonekana kuwashangaza watu wengi wa eneo hilo.
Mama huyo mwenye watoto saba akizungumza na waandishi wa habari amesema mwezi Novemba mwaka 2023 alianza kujihisi ana ujauzito kwani alikuwa na dalili zote zinazoonesha kuwa yeye ni mjamzito japo alikuwa hajawahi kwenda kupima.
"Ilipofika mwezi wa kumi na moja mwaka jana nikaacha kuona siku zangu nikakaa sasa jana nikiwa nafunga biashara zangu usiku tumbo likaanza kuniuma nikajikaza kufika nyumbani likaendelea kuniuma sana nikawa nimemuita jirani yangu angalau aweze kunipeleka hospitali"
"Yule jirani yangu alipofika akanikuta niko katika harakati ya kusukuma akaniambia basi vua hizo nguo nikavua baada ya kusukuma mara moja mara mbili mara ya tatu ndio yakatoka yale majitu sasa akawa amemulika na tochi sasa akaona kale kandege kametanguliza mdomo na miguu" ameeleza mwanamke huyo.
NIPASHE