Gen Z Kenya haijaisha mpaka iishe wapanga maandamano upya.
Joyce Shedrack
July 21, 2024
Share :
Baadhi ya wananchi Nchini Kenya wakiongozwa na kundi la Vijana Gen Z wamepanga kufanya maandamano ya amani kwa mara nyingine Nchini humo kwa ajili ya kupinga Uteuzi wa Mawaziri 6 waliorejeshwa na Rais William Ruto kwenye orodha ya Mawaziri 11 walioteuliwa na Rais huyo siku ya ijumaa.
Tarehe 19 mwezi huu Rais Ruto alitangaza orodha ya kwanza ya majina 11 ambayo yataenda bungeni kukaguliwa na kupitishwa kwa nafasi ya baraza la mawaziri wa Nchi hiyo.
Ikumbukwe kuwa Rais huyo alifanya hivyo ikiwa ni baada ya wiki moja tangu avunje baraza la mawaziri 21 kutokana na shinikizo la wananchi wanaotaka mabadiliko ya serikali.
Hata hivyo baada ya kuvunja baraza hilo na kuliunda upya bado baadhi ya wakazi wa Nchi hiyo wameonekana kutokuridhishwa na majina yaliyorejeshwa tena kwenye uongozi huku wakipanga kufanya maandamano julai 23 siku ya jumanne.
Majina yaliyorejeshwa kwenye uongozi na Rais Ruto ni Kithure Kindiki, Aden Duale, Alice Wahome , Rebecca Miano, Davis Chirchir na Soipan Tuya.