pmbet

Genge la El Mencho laanza kulipiza kisasi dhidi ya serikali Mexico kisa kuuwa kwa kiongozi wao

Sisti Herman

February 23, 2026
Share :

 

Baada ya Oseguera Cervantes maarufu kama “EL Mencho”, Mfanyabiashara mkubwa wa kuuza dawa za kulevya aliyekuwa akisakwa zaidi Nchini Mexico huku akiliongoza kundi la ‘Jalisco New Generation Cartel’ Nemesio “El Mencho” kuuawa katika operesheni ya kijeshi Nchini Mexico baada ya Serikali ya Marekani kutoa msaada wa kijasusi, Watu wanaoaminika kuwa Wanachama wa Genge hilo ‘Vijana wa El Mencho’ limefanya machafuko makubwa kwa kuchoma na kuteketeza Mabasi na Biashara mbalimbali huku wakipambana na Vikosi vya usalama.

Video inayosambaa kwenye Vyombo vya habari kwa sasa inaonyesha moshi ukisambaa kutoka uwanja wa ndege wa Puerta Vallarta ambapo Watalii wameonekana wakikimbia na kutafuta hifadhi baada ya moshi na vurugu kuzuka huku safari za ndege kuelekea Mji Mkuu wa Jimbo la Jalisco zikisitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ikiwahimiza Raia wa Marekani katika sehemu mbalimbali za Mexico kutafuta sehemu zilizo salama na kutulia.

Mike Vigil, Mkuu wa zamani wa Operesheni za Kimataifa wa DEA amenukuliwa akisema kuwa operesheni hiyo ya kijeshi ilikuwa moja operesheni muhimu zaidi katika hatua zilizochukuliwa kwenye historia ya biashara ya dawa za kulevya.

Wakati wa operesheni hiyo Askari walifyatua risasi na kuua Watu wanne katika eneo la tukio ambapo Watu wengine watatu akiwemo Oseguera Cervantes, walijeruhiwa na baadaye kufariki huku Wawili wengine wakikamatwa na magari ya kivita na kurusha roketi.

Mauaji ya Mfanyabiashara huyu mwenye nguvu ya dawa za kulevya yalisababisha vizuizi viwekwe barabarani kwa saa kadhaa ikiwemo magari yanayowaka moto katika eneo la Jalisco na Majimbo mengine zikiwa mbinu za kawaida zinazotumika na Magenge ya kihalifu kuzuia shughuli za kijeshi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet