Genge la wahalifu Haiti, lavamia kituo cha Polisi na kuchinnja Askari
Eric Buyanza
July 3, 2024
Share :
Huko nchini Haiti, Genge la wahalifu limevamia kituo cha polisi na kuchinja idadi kubwa ya askari waliokuwa kituoni hapo kwa mujibu wa ripoti.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star wanachama wa genge hilo linaloongozwa na mbabe maarufu nchini humo, Jimmy "Barbecue" Cherizier walishambulia kituo hicho kwenye kitongoji cha Gressier kwenye mji wa Port-au-Prince, wakitumia silaha nzito na kuua takriban askari 20.