pmbet

Georgina aibuka na vazi la Ronaldo kwenye Fashion Show

Sisti Herman

March 3, 2024
Share :

Mpenzi wa mchezaji wa Al Nassr na Ureno Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez ameonesha kumsapoti, na kumpa heshima mpenzi wake huyo kwa kuvalia vazi lililoandikwa jina la Ronaldo katika maonesho ya mavazi ya ‘Vetements Fall/Winter’ yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Paris.

Georgina alivaa gauni jekundu yenye jina la mpenzi wake pamoja na namba saba ambayo mchezaji huyo anayetajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora muda wote amekuwa akiivaa toka yupo Man Utd, Real Madrid, Juventus, Al Nassr hadi timu ya Taifa Ureno.

Cristiano Ronaldo na Georgina Rodriguez wapo katika uchumba kwa muda mrefu, wanaishi na mrembo huyo amembariki Ronaldo watoto wawili kati ya watano wa Cr7.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet