Geremi Njitap adai talaka baada ya kubaini yeye si baba wa watoto wake!
Eric Buyanza
March 25, 2024
Share :
Kiungo wa zamani wa Real Madrid na Chelsea, Geremi Njitap, ameomba talaka mahakamani aachane na mke wake Toukam Fotso Laure Verline, aliyeishi nae kwenye ndoa kwa miaka 12 baada ya kubaini yeye si baba mzazi wa watoto wake wawili (Mapacha).
Hilo limejiri baada ya majibu ya kipimo cha DNA kubaini kuwa baba mzazi wa watoto hao ni aliyekuwa mume wa mke wake kipindi cha nyuma (mtaliki wa mkewe).
Inaelezwa kuwa mpaka wakati uchunguzi wa DNA unaenda kufanyika, mwanasoka huyo Cameroon alikuwa akiamini watoto hao mapacha ni wake.