Giovanni Van Bronckhorst ajiunga na Liverpool kama kocha msaidizi
Eric Buyanza
July 2, 2025
Share :
Liverpool wamethibitisha kuwa Giovanni van Bronckhorst amejiunga na benchi la ukufunzi la Arne Slot kama kocha msaidizi.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi amewahi kuinoa Feyenoord, Guangzhou R&F, Rangers na Besiktas.
Xavi Valero nae amerejea Liverpool kama mkuu wa ukufunzi wa makipa wa kikosi cha kwanza, akitokea West Ham ambapo alihudumu kwa miaka saba.