Goli bora la Kombe la Dunia limetokea Afrika kwa kina Vozinha alifungwa Messi
Joyce Shedrack
July 29, 2026
Share :
Beki wa Timu ya Taifa ya Cabo Verde, Sidny Lopes Cabral, ametwaa tuzo ya Bao Bora la Kombe la Dunia 2026 baada ya bao lake la kuvutia dhidi ya Argentina kuchaguliwa kuwa bora zaidi na mashabiki kupitia kura za FIFA.

Cabral aliandika historia kwa kufunga bao la kusawazisha kwa shuti kali lililopinda na kutinga kona ya juu ya lango dhidi ya mabingwa watetezi Argentina katika hatua ya 32 Bora.
Cabo Verde iliondolewa kwenye michuano hiyo kwa kufungwa mabao 3-2, bao hilo limebaki kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya mashindano hayo.
Bao lake limepongezwa na wadau wengi wa soka duniani kutokana na ubora wake wa kiufundi, nguvu na utulivu aliouonyesha wakati wa kulifunga.





