Gor Mahia kukipiga na Simba kumuenzi Raila Odinga
Sisti Herman
November 2, 2026
Share :

Ripoti kutoka nchini Kenya zimesema kuwa klabu kubwa nchini humo Gor Mahia imepangwa kukabiliana na klabu kubwa ya Tanzania, Simba SC, katika michuano inayopendekezwa ya 'Raila Odinga Cup' mnamo tarehe 15 Novemba 2026, ikiwa ni maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Waziri Mkuu na mlezi wa Gor Mahia, Raila Odinga.
Simba SC wapo kwenye mpango wa kusafiri kuweka kambi fupi nchini humo wakati huu wa mapumziko ya ligi mbalimbali kupisha mechi za timu za taifa kwenye kalenda ya FIFA ya mwezi Novemba.





