Gor Mahia wajifunza kwa Yanga
Sisti Herman
July 16, 2024
Share :
Baada ya kukamilisha dili la kutengenezewa jezi na mbunifu maarufu wa mavazi nchini Tanzania Sheria Ngowi, viongozi wa klabu ya Gor Mahia ambao pia ni mabingwa ligi kuu nchini Kenya na wawakilishi wa nchi hiyo kwenye michuano ya CAF wametembelea makao makuu ya klabu hiyo kwaajili mambo mbalimbali ikiwemo kujifunza kwao.
Viongozi wa Gor Mahia wakiongozwa na Mwenyekiti wa klabu Ambrose Richier waliopokelewa na Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said.