pmbet

Gordon asema Uingereza hawakumthamini, sasa alinganishwa na Lamine

Eric Buyanza

October 7, 2026
Share :

Kauli maarufu ya kituo kimoja cha habari za michezo iliyodai kuwa mapinduzi ya kiwango cha winga Anthony Gordon "yatakuja kusomwa na kufundishwa kwa miaka mingi ijayo," sasa imeonekana kuwa ukweli mtupu, huku nyota huyo akizidi kuwasha moto mkali akiwa na klabu yake mpya ya FC Barcelona pamoja na timu ya taifa ya Uingereza.

 

Gordon, ambaye alihamia FC Barcelona msimu huu wa kiangazi kwa ada ya pauni milioni 69.3 akitokea Newcastle United, amebadilika kabisa chini ya kocha Hansi Flick, akionyesha ukomavu mkubwa wa kiufundi na akili ya soka inayowaacha midomo wazi wachambuzi wengi barani Ulaya.

 

Katika mapumziko haya ya kimataifa, Gordon ameibuka kuwa mchezaji tegemeo zaidi wa Uingereza chini ya kocha mpya Thomas Tuchel. Winga huyo amefanikiwa kufunga mabao katika mechi tatu mfululizo za UEFA Nations League dhidi ya Hispania na Czech Republic, kabla ya October 3 kutoa asisti na kufunga bao lingine katika ushindi wa kihistoria wa 7-0 dhidi ya Croatia.

 

Tangu atue nchini Hispania, Gordon amekuwa mashine ya kutengeneza mabao. Katika mechi yake ya kwanza kabisa ya ushindani akitokea benchi dhidi ya Elche, alitoa asisti mbili ndani ya dakika nne tu—hatua ambayo haikuwahi kufanywa na mchezaji yeyote mpya wa Barcelona kwa miaka 15 iliyopita. Hadi sasa, tayari ana asisti tano katika mechi saba alizocheza.

 

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Croatia, Gordon alikiri kuwa mfumo wa soka wa Hispania umemsaidia kuonyesha uwezo wake halisi, huku akitupa dongo kwa mashabiki wa nyumbani.

 

"Nikiwa Uingereza, watu walikuwa wananiheshimu tu kwa sababu nina kasi na uwezo wa kukimbiza mabeki, lakini hawakuwahi kuheshimu ubora wa kiufundi na akili ya soka ninayocheza nayo. Sasa nikiwa Barcelona, nadhani watu wameanza kuona kuwa mimi si mchezaji wa kukimbia tu uwanjani," alisema Gordon.

Kiwango chake kikubwa kimepelekea kocha wa timu ya taifa ya Czech, Santi Denia, kumtaja Gordon kuwa kwa sasa yuko kiwango kimoja na staa mwingine wa Barcelona, Lamine Yamal, kauli ambayo imezua mijadala mizito kwa mashabiki wa soka mtandaoni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet