pmbet

Greenwood wa Man Utd awa mchezaji bora wa msimu Getafe

Sisti Herman

May 29, 2024
Share :

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Mason Greenwood ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Getafe ya ligi kuu Uhispania maechagualiwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa 2023/24 wa Getafe baada ya kucheza kwa kiwango kikubwa sana.

Akiwa na Getafe msimu huu kinda huyo amefunga magoli 8 na asisti 6 huku akiwa mchezaji wa pili kucangia idadi kubwa ya magoli baada ya Broja Mayoral ambao kwa pamoja waliisaidia Getafe kuwa nafasi ya 12 kwenye La Liga.

Greenwood alikuwa na skendo nyingi za unyanyasaji kwenye mahusiano yake kuanzia mwaka 2022 baada ya kushinda kesi msimu jana aliamua kujiunga na Getafe baada ya Manchester United kumfungia vioo.

Licha ya kuwa na kiwango bora Manchester United haitazamii kumrejesha bali imemuweka kwenye dirisha la usajili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet