"GSM amekubali kujenga uwanja wa kisasa" - Ali Kamwe
Sisti Herman
February 11, 2024
Share :
Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ali Shaban Kamwe amethibitisha kuwa mdhamini na mfadhili wa klabu hiyo Gharib Said Mohammed (GSM) amekubali kuijengea klabu hiyo uwanja wa kisasa.
“Baada ya majadiliano ya muda mrefu na Rais Eng. Hersi Said, Leo mdhamini na mfadhili wa klabu ya Yanga, Gharib Said Mohammed (GSM) amekubali kujenga uwanja wa kisasa wa Yanga makao makuu ya klabu Jangwani” aliandika hivyo Kamwe kupitia mitandao yake ya kijamii.
GSM ameridhia ombi hilo leo klabu hiyo ikisherekea kutimiza miaka 89 tangu kuanzishwa kwake.