GSM wamwaga fedha Yanga kupitia vinywaji
Sisti Herman
July 30, 2024
Share :
Kampuni ya GSM Group imeidhamini rasmi klabu ya Yanga kupitia bidhaa zao mpya za Vinywaji "GSM Baverages" kwa mkataba wa miaka mitano (5) wenye thamani ya Tsh Bilioni 1.
“Kwa niaba ya GSM Group tunayo furaha ya kutangaza rasmi kuwa tumepanua wigo wa mahusiano yetu na klabu ya Yanga SC, tunatangaza rasmi kuwa kampuni mpya ya vinywaji ya GSM imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu ya Yanga SC, na mkataba huu una thamani ya Tsh bilion 1” alisema Benson Mahenya CEO wa GSM Group wakati wa hafla hiyo.
“Tunashukuru sana Uongozi wa GSM Group kwa kutambua umuhimu wa kuongeza nguvu ya udhamini kwa klabu yetu, Kampuni hii ya vinywaji visivyo na kileo kama juisi, soda na maji itakuwa sehemu ya wadhamini wetu kwa kipindi hicho cha miaka mitano” aliongeza Simon Patrick Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga SC.