Guardiola adokeza, Kyle Walker aweza kurejea dhidi ya Real Madrid
Eric Buyanza
April 15, 2024
Share :
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amedokeza kwamba Kyle Walker anaweza kurudi uwanjani kwa ajili ya mchezo mgumu wa Jumatano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid.
Walker hajaingia uwanjani tangu alipopata majeraha kwenye misuli ya paja alipokuwa akiichezea timu yake ya taifa (England) katika mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil mwezi uliopita.