pmbet

Guardiola ahimiza wachezaji kugomea ratiba za FIFA

Sisti Herman

January 1, 2024
Share :

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameunga mkono tishio la Chama cha Wanasoka wa Kulipwa England (PFA) la kuishtaki Shirikisho la Soka duniani (FIFA) kutokana na kalenda yao yenye ratiba nyingi kuonekana inahatarisha afya za wachezaji.


Mkuu wa chama hicho, Maheta Molango alifichua wanachama wake wanataka kuchukua hatua za kisheria, baada ya mipango ya kuongeza mashindano mapya ya kimataifa, huku kukiwa na muda mchache wa mapumziko kwa wachezaji.

Guardiola alipendekeza mapema msimu huu wachezaji wanapaswa kufikiria kugoma, ili kuonyesha kutoridhika na ratiba nyingi za mechi. Kocha huyo alisisitiza hajapendezwa na ratiba nyingi kubana kwenye kalenda ya FIFA, kwani wataathirika zaidi na ongezeko la mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia la Klabu.

“Naelewa kabisa, alisema. “Ni wao tu wanaweza kubadilisha kitu (wachezaji). Nimezungumza sana, tuna mechi nyingi sana. Shida ni tuna wiki tatu tu za likizo katika msimu wa joto. Haitoshi kujiweka fiti. Angalia idadi ya majeruhi inaongezeka pia.”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet