pmbet

Guardiola akataa kadi nyekundu ya Szoboszlai"Toa tu bao iwe 1-3".

Joyce Shedrack

February 9, 2026
Share :

Kocha Mkuu wa Manchester City Pep Guardiola akitoa maoni yake kuhusu kadi nyekundu aliyopata mchezaji wa Liverpool Dominick Szoboszlai kwenye mchezo wa jana amesema ni bora mwamuzi wa mchezo angewapa goli la 3 mechi iishe 3-1 na kisha asingetoa kadi nyekundu kwa nyota huyo.

Dominik Szoboszlai Liverpool red card fume cleared up as Premier League  explain decision - Liverpool Echo

Manchester City walipata goli la 3 lililofungwa na Cherki kwenye mchezo huo ulioisha 2-1 dhidi ya Liverpool kabla ya goli hilo kukataliwa na mwamuzi kwa msaada wa VAR kutokana na rafu aliyocheza Dominick Szoboszlai kwa Erling Haaland kabla ya goli hilo kuzama nyavuni.
 

“Akili ya kawaida, sivyo Tulishinda mechi, na sasa Szoboszlai hawezi kucheza kwa sababu amesimamishwa. Najua alimvuta Haaland"
 

“Lakini ni mara ngapi kuvutana kunatokea kwenye mechi na waamuzi wanasema, ‘Endeleeni kucheza, endeleeni kucheza, endeleeni kucheza!’”
 

“Katika nchi hii kwenye ligi hii, IMEKUWA hivyo KILA MARA‘Cheza, cheza!’ Kwa hiyo toa tu bao, iwe 1-3, Szoboszlai anaweza kucheza, na sisi tunafurahi!”Alisema Halaand.

 

Erling Halaand naye ametoa maoni yake huku akisisitiza kuwa mwamuzi angetoa tu goli bila kutoa kadi nyekundu kwa Szoboszlai.

 

“Mwamuzi lazima afuate sheria Lakini mwishowe, kwa kweli NAJISIKIA VIBAYA kwa Dominik Szoboszlai sasa, anapata adhabu ya kutocheza mechi 3... Toa tu bao, usitoe kadi nyekundu! Rahisi hivyo. Lakini nadhani ni sheria, ndivyo ilivyo tu.” Amesema Haaland.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet