Guardiola akiri kukosekana kwa Kovacic ni pigo kubwa
Eric Buyanza
February 14, 2026
Share :

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amefichua kwamba kukosekana kwa Mateo Kovacic kwa muda mrefu kutokana na majeraha kumekuwa ni hasara kubwa kwenye kikosi chake.
Kovacic amecheza mechi mbili pekee tangu Oktoba na alionekana mara ya mwisho kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Villarreal.
"Ninamkumbuka sana, uwezo wake katika pasi fupi fupi na tunapocheza bila mawinga wazuri, na wachezaji wengi ndani," Guardiola alisema.
"Anajisikia vizuri sasa ikilinganishwa na upasuaji wa kwanza na tunatumai anaweza kutusaidia katika sehemu ya mwisho ya msimu."





