Guardiola alivyomfanya Messi kuwa Mshambuliaji Kivuli 'False 9'
Sisti Herman
May 16, 2024
Share :
FALSE NUMBER 9
False 9 au mshambuliaji kivuli sio neno geni kwenye masikio ya mashabiki na wafuasi wa mpira wa miguu, ni moja kati ya maneno yanayotumiwa sana na wachambuzi wa mchezo huu
Maana ya False 9
Neno "False 9" limetokana na nafasi ya mshambuliaji wa kati uwanjani kati ya wachezaji 11, ambapo mchezaji namba 9 huwa mshambuliaji wa kati na mshambuliaji kivuli huwa mshambuliaji wa kati mwenye majukumu tofauti na yale ya mshambuliaji wa kati wa kawaida kwani kuna kuna wakati hutoka kwenye eneo lake asilia na kuwa kama kiungo
Historia ya False 9
Mshambuliaji kivuli alinza kutumika mara ya kwanza miaka ya 1890s kwenye klabu ya Corinthians ya Brazil pale ambapo mshambuliaji wa kati alikua akirudi hadi eneo la kiungo na kupokea mashambulizi ili awatengenezee nafasi Washambuliaji wa pembeni
Pia mshambuliaji kivuli alitumiwa miaka ya 1920s kwenye klabu ya River plate ya Argentina na miaka ya 1930s timu ya Taifa ya Austria ilipomtumia mshambuliaji Mathias Sindelar na aina hii ya uchezaji ikaendelea kuchezwa hadi wanasoka wa kisasa walipokuja na neno "False 9"
Majukumu ya False 9 timu anayochezea inapo miliki mpira
Majukumu ya mshambuliaji kivuli timu yake inapomiliki mpira ni kufanya mikimbio yenye ulekeo tofauti na ulekeo wa goli ambalo timu yake inalishambulia, yaani kurudi hadi katikati ya viungo na mabeki wa timu pinzani ili aweze kupokea mipira na kuweza kuwachezesha Washambuliaji wenzake na mikimbio yake inakua inaacha maswali kwa mabeki, wamfuate na kuacha nafasi au wamuache na awe huru kupokea na kutengeneza mashambulizi kwa wenzake
Majukumu ya False 9 timu anayochezea isipokua kwenye umiliki wa mpira
Majukumu ya False 9 timu yake isipokua kwenye umiliki wa mpira hautofautiani na mshambuliaji wa kati wa kawaida, kwa atalazimika kukaba kwenye mstari wa ushambuliaji "counter pressing" ili wachezaji wa timu pinzani wasianzishe mashambulizi ya kishtukiza na mpira unapokua eneo la viungo hulazimika kurudi eneo la Kati kuongeza idadi ya watu na kulazimisha mpira kupita pembeni "numerical advantage"
Sifa za mchezaji kuwa False 9
Ili mchezaji aweze kutimiza majukumu ya kuwa mshambuliaji kivuli ni lazima awe na ubora mkubwa sana wa kumiliki mpira, awe na uwezo wa kupiga chenga ili kuepuka shinikizo "pressure" pale anaposhinikizwa kwani eneo anayocheza linakuwa na idadi kubwa ya wachezaji wa timu pinzani "between the lines" pia anatakiwa awe na mguso wa kwanza bora "first touch" ambayo huupeka mpira ulekeo mgumu kwa mpinzani kuupokonya na kuweza kukokota na kuweza kuwatengenezea wenzake nafasi au kufunga
Faida ya timu kutumia False 9
Faida ya timu kutumia mshambuliaji kivuli ni Washambuliaji wenzake kufaidika na mikimbio yake ambapo mebeki wa timu pinzani huweza kumfuata kumkaba na kuacha nafasi ambayo wenzake huishambulia lakini pia asipofuatwa na mabeki wa timu pinzani huweza kuwa huru na kuwatengenezea nafasi za kufunga wenzao
Athari za timu kutumia False 9
Athari za timu kutumia mshambuliaji kivuli ni pale ambapo mshambuliaji aliyepewa majukumu kutokua na sifa na vigezo vya kuwa False 9 kwani anaposhinikizwa kupoteza mipira anakua na mguso wa kwanza hafifu na pia kuwa na uwezo mdogo wa kutengeneza nafasi kwa wenzake
Mifano ya wachezaji na Makocha wanaotumia False 9
Mchezaji maarufu kucheza kama mshambuliaji kivuli ni Lionel Messi hasa alipokua chini ya Pep Guardiola lakini pia Karim Benzema chini ya Zenedine Zidane, Roberto Firminho chini ya Klopp na pia viungo wa Manchester City kama Kelvin De Bruyne,Bernado Silva, Ilkay Gundogan na Phil Foden chini ya Pep Guardiola