Guardiola alivyotumia Mbinu za Ten Hag kuifunga Arsenal Fainali Carabao Cup
Sisti Herman
March 23, 2026
Share :

Utangulizi
Manchester City jana ilitawazwa kuwa mabingwa wa EFL Cup (Carabao Cup) ikiifunga Arsenal 2-0, magoli ya City yakifungwa na beki wa kushoto Nico O'Reilly.

Takwimu za mchezo zinaonyesha kuwa City waliutawala mchezo kwa umiliki wa mpira wa 62% huku wakitengeneza nafasi nyingi za kufunga ambapo kati ya mashuti 10 waliyopiga mawili yalilenga lango na kupata magoli mawili.
Pep Guardiola alivyotumia Mbinu za Eric Ten Hag.
Kwenye mchezo huo City ili kutawala mchezo ilihakikisha inazuia kwa Arsenal kutoweza kumili mpira kwa asilimia kubwa ambapo ilianza kuzuia Arsenal kuanzia mbele kwa muundo wa 4-2-4 na kuwalazimisha mabeki wao kupiga mipira mirefu badala ya kupita njia za kati na pembeni, huku wakihakikisha hiyo mipira ya juu mabeki wao wanashinda mapambano ya juu.
Mbinu za Ten Hag zilikuwaje?
Kwenye fainali ya Kombe la FA mwaka 2024, Kocha wa Manchester United Eric Ten Hag alitumia mbinu hizo za uzuiaji na kutwaa taji mbele ya Guardiola kwa ushindi wa goli 2-1.
Muundo wa Ten Hag ulikuwaje?

Man City waliokuwa wakitumia mfumo wa 4-2-3-1, wakiwa na mpira kwenye theluthi yao ya kwanza (Build up phase) walijenga shambulizi wakiwa na umbo la 3-4, Man United walizuia kuanzia mbele kwa shinikizo dogo na muundo wa 4-2-4 (high block) ambapo;
- Mstari wa kwanza wa uzuiaji wa United ulikuwa na watu wanne, kati Bruno & McTominay na pembeni Rashford & Garnacho huku nyuma tao kukiwa na viungo wawili Mainoo na Amrabat
- Mstari wa kwanza wa ujenzi wa shambulizi wa City ulikuwa na Kipa Ortega, Stones na Ake huku mbele yao kukiwa na mstari wa watu wanne wanaoweza kuendeleza shambulizi, pembeni Walker & Gvardiol na kati Rodri na Kovacic
Mkakati wa uzuiaji ulikuwaje?
Wachezaji wanne wa mbele wa Man United walihakikisha wanakuwa sambamba pamoja wakizuia na kukata mawasiliano na kuzuia uendelezwaji wa shambulizi (build up progressions) kutoka wachezaji watatu watatu Man City wanaojenga shambulizi kutokea nyuma (building up from back) kwenda kwa wachezaji wa pembeni au katikati

Hali hii iliwalazimisha Wachezaji hao kupita njia za juu na kurahisisha uzuiaji wa Man United kwani wachezaji wa nyuma walikuwa na jukumu la kuhakikisha wanashinda mipira yote ya kupambania juu na chini kisha kurejesha umiliki na wa mpira kwao nyakati nyingi hali iliyowapa utawala wa mchezo.
Guardiola akautumia dhidi ya Arsenal.
Kwasababu silaha kubwa ya Arsenal wakati wa ujenzi wa shambulizi ni kuanzia nyuma kwa kipa wao ili kuwavuta wapinzani kushawishika kuwafuata kuwashinikiza kukosea na kuwapora mpira, kisha wao kutoka kwa wachezaji wao kupata nafasi katikati ya mistari uzuiaji huku wachezaji wao wakibadilishana nafasi ili kuwavuruga wapinzani, Man City hawakuingia kwenye mtego huo
Walichokifanya kuzuia kuanzia mbele kwa shinikizo dogo (high block) wakifunga njia badala ya shinikizo la juu kwa Arsenal kukosea (high press) ili kuwapora mpira
Arsenal wakiwa na mpira kwenye theluthi yao ya kwanza (Build up phase), Man City walizuia kuanzia mbele kwa shinikizo dogo na muundo wa 4-2-4 (high block) ambapo;
- Mstari wa kwanza wa uzuiaji wa United ulikuwa na watu wanne, kati Haaland & Cherki na pembeni Dorku & Semenyo huku nyuma tao kukiwa na viungo wawili Rodri na Bernado
- Mstari wa kwanza wa ujenzi wa shambulizi wa Arsenal ulikuwa na Kipa Kepa, Gabriel na Saliba huku mbele yao kukiwa na mstari wa watu wanne wanaoweza kuendeleza shambulizi, pembeni Ben White & Hincape na kati Zubimendi na Rice
Mkakati wa uzuiaji ulikuwaje?
Wachezaji wanne wa mbele wa City walihakikisha wanakuwa sambamba pamoja wakizuia na kukata mawasiliano na kuzuia uendelezwaji wa shambulizi (build up progressions) kutoka wachezaji watatu watatu Arsenal wanaojenga shambulizi kutokea nyuma (building up from back) kwenda kwa wachezaji wa pembeni au katikati.
Hali hii iliwalazimisha Wachezaji kupiga pasi ndefu ili kupita njia za juu na kuingia kwenye mtego wa City kwani wachezaji wa nyuma walikuwa na jukumu la kuhakikisha wanashinda mipira yote ya kupambania juu na chini kisha kurejesha umiliki na wa mpira kwao nyakati nyingi hali iliyowapa utawala wa mchezo.
Mkakati huo ulisaidia upatikanaji wa goli la pili la City.





