Guardiola aogopa kujibu swali hili!
Eric Buyanza
December 4, 2023
Share :
Baada ya maamuzi yaliyozua utata kwenye dakika za mwisho za mchezo wa ligi kuu England kati ya Manchester City dhidi ya Totenham Hotspurs, kocha wa Manchester City Pep Guardiola amegoma kutoa maoni kuhusu jambo hilo akikiri kuogopa yaliyomkuta kocha wa Arsenal Mhispaniola mwenzake Mikel Arteta baada ya kukumbwa na adhabu za kukiuka kanuni kuhusu kuwasema vibaya waamuzi wa mchezo.
"Swali lingine tafadhali, sitaki kutoa maoni kama ya Arteta" alisema Pep huku akicheka baada ya kuulizwa kuhusu hilo na mwandishi wa kituo cha habari cha Sky Sports cha Uingereza chenye haki ya matangazo huo.
Wakati mchezo ukielekea ukingoni, dakika ya 6 ya nyongeza baada ya dakika 90 za mchezo, City wakishambulia, Erling Halland akiwa na mpira alichezewa rafu na mchezaji wa Spurs lakini hakuanguka na kuathiri mwenendo wa shambulizi baada ya hapo akatoa pasi kwa Jack Grealish aliyekuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga ndipo Mwamuzi akapuliza kipenga kufidia madhambi aliyochezewa Halland.
Tukio hilo lilizua taharuki na mshangao kwa watazamaji, wachezaji na wengine wote walioshudia, mchezo ulimalizika kwa sare ya 3-3, Spurs wakiwa ugenini.