pmbet

Guardiola kuwakosa Walker na Stones kwenye game na Arsenal

Eric Buyanza

March 29, 2024
Share :

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amethibitisha kuwa walinzi wake wawili Kyle Walker na John Stones watakosa mechi ya Jumapili ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Arsenal kwenye Uwanja wa Etihad.
 

Walker aliumia wikiendi iliyopita akiwa na timu ya taifa ya Uingereza ilipocheza na Brazil na wakapoteza kwa bao 1-0.
 

Katika mchezo huo Walker alilazimishwa kutoka nje kwenye dakika ya 19 baada ya kupata jeraha kwenye misuli ya paja.
 

Stones naye alicheza dakika zote 90 dhidi ya Brazil, lakini alidumu kwa dakika 10 tu katika sare ya 2-2 dhidi ya Ubelgiji baada ya kupata tatizo la paja wiki hiyohiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet