Guardiola kwenye mazungumzo ya kuinoa Italia
Eric Buyanza
July 22, 2026
Share :
Rais wa Shirikisho la Soka Italia (FIGC), Giovanni Malagò, amethibitisha kuwa kumekuwa na mazungumzo na Pep Guardiola kuhusu uwezekano wa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya taifa ya Italia.
Guardiola aliondoka Manchester City msimu huu wa kiangazi baada ya kuitumikia kwa mafanikio makubwa kwa miaka 10, akitwaa mataji 6 ya Ligi Kuu England, 3 ya FA Cup, 5 ya Carabao Cup na 1 la UEFA Champions League.
Kwa sasa, Italia haina kocha tangu Gennaro Gattuso ajiuzulu mwezi Aprili kufuatia taifa hilo kushindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya tatu mfululizo.






