Guede anukia Singida, awapisa Dube na Baleke Jangwani
Sisti Herman
July 9, 2024
Share :
Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Joseph anatwajwa na vyanzo mbalimbali vya habari kuwa kwenye mazungumzo na klabu ya Singida Black Stars kwaajili ya kujiunga nao.
Mshambuliaji huyo alimaliza na mabao sita katika Ligi Kuu na matatu ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita akiwa na kikosi cha Yanga anatajwa kuwapisha washambuliaji wapya.
Guede alijiunga na Yanga katika dirisha dogo la Januari akitokea Tuzlaspor FC ya Uturuki akiitumikia kwa miezi sita na anatajwa ni kati ya nyota wa kigeni walioachwa kikosini, ili kupisha mastaa wapya akiwamo Jean Baleke anayeenda kuchukua nafasi yake eneo la ushambuliaji.
Awali mshambuliaji huyo, ilielezwa alikuwa na nafasi kubwa ya kubaki Yanga kutokana na viongozi kutofautiana juu ya kutemwa kwake na hasa baada ya kuelezwa kocha mkuu, Miguel Gamondi hakutaka aondoke kwani anamkubali sana, lakini kwa sasa inasemkana anaondoka akimpisha Baleke aliyepewa mwaka mmoja.