"Guede kufunga ilikuwa suala la muda tu" - Ali Kamwe
Sisti Herman
February 21, 2024
Share :
Mara baada ya mshambuliaji wa Yanga Joseph Guede kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa goli 5-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora wa kombe la shirikisho la ASFC, Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kuwa suala mshambualiaji huyo kufunga lilisubiri muda tu ila waliamaini kuwa utafika kwasababu ya namna anavyocheza mazoezini na kwenye mechi zake chache alizoanza.
“Nliwaambia siku Guede akifunga halitakuwa goli mmoja, ni mawili na kuendelea kwasababu sisi tunaona ubora wake akiwa mazoezini tunaona nafasi anazotengeneza na nafasi anazotengenezewa suala la kufunga goli tulijua litakuja tu, ameshaizoea ligi na leo unaona mipira miwili ya vichwa yote kamba" alisema Ali Kamwe aliponukuliwa na PM Sports.
kwasisi tunaojua mpira, washambuliaji wetu wamefunga magoli matatu kwa maana ya Guede mawili na Mzize moja maana yake washambuliaji wetu wapo kwenye moto kwelikweli na kuelekea kwenye mchezo mkubwa wikiendi dhidi ya CR Belouizdad una uhakika viungo wanafungawashambuliaji wanafunga, maana yake una uhakika wa magoli” alihitimisha kwa kutamba Ali Kamwe.
Ali Kamwe amesema hayo kwenye mahojiano na PM Sports mara baada ya mchezo huo uliochezwa jana kwenye uwanja wa Azam Complex.