Gwiji wa Arsenal ageuka mbogo kisa ubingwa wa AFCON 2025.
Joyce Shedrack
March 18, 2026
Share :
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na Man City raia wa Ufaransa, Samir Nasri, ameikosoa vikali Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka (CAF) kufuatia uamuzi wake wenye utata wa kuipatia Morocco ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Senegal katika fainali ya AFCON 2025.

Uamuzi huo, uliotolewa na Kamati ya Rufaa ya CAF baada ya Senegal kuonekana kuwa walijiondoa uwanjani na hivyo kupoteza mechi, umeendelea kuzua mjadala mkali katika ulimwengu wa soka.
Nasri, akizungumza kuhusu tukio hilo, hakuficha hisia zake, akieleza hali hiyo kuwa ya ovyo na iliyoshughulikiwa vibaya.
“Mara nyingine watangaze tu mwaka 2035 pia hii ni kinyume kabisa na haki ni upuuzi, Wachezaji wa Senegal tayari walirudi nyumbani na kombe kusherehekea ushindi wao alafu leo mnawapokonya Sasa tufanye nini? Tulipe Morocco kombe?”
"Shirikisho la Soka la Afrika limefanya jambo lisilo na maana kabisa,limefanya kituko kabisa,” amesema Nasri.





