Gwiji wa Man U atimuliwa kwenye majukumu ya Taifa lake.
Joyce Shedrack
March 7, 2026
Share :
Gwiji wa Manchester United ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Trinidad and Tobago Dwight Yorke amepewa mkono wa kwaheri baada ya kushindwa kulisaidia Taifa hilo kufuzu Kombe la Dunia 2026.
Mshambuliaji huyo wa zamani, ambaye bado anakumbukwa sana katika uwanja wa Old Trafford kwa mchango wake katika msimu wa kihistoria wa treble wa mwaka 1999, ameondoka baada ya mazungumzo ya mkataba kuvunjika.

Yorke alichukua nafasi ya ukocha mnamo Novemba 2024 akiwa na matumaini makubwa ya kuipeleka nchi yake kwenye jukwaa la dunia, akitarajia kurudia mafanikio aliyopata akiwa mchezaji wakati wa safari yao ya kihistoria ya Kombe la Dunia mwaka 2006.
Hata hivyo, timu hiyo iliishia nafasi ya tatu katika kundi lao la kufuzu, jambo lililosababisha kushindwa kwao kufuzu na hatimaye kupelekea kuondoka kwake.





