pmbet

Gym inatoa zawadi ya gari kwa atakayeweza kupunguza kilo 45

Eric Buyanza

November 10, 2025
Share :

Jumba moja la mazoezi ya viungo (Gym) lililoko katika Jiji la Binzhou, Mkoa wa Shandong nchini China limetangaza kutoa zawadi ya gari aina ya Porsche Panamera kwa mtu atakayeweza kupunguza kilo 45 ndani ya miezi mitatu.

Washiriki walio tayari kushiriki watahitajika kujisajili kwa kulipa ada ya Yuan 10,000 (sawa na Shilingi Milioni 3.4 za kibongo) na watapimwa uzito kabla ya kuanza kwa mchakato wa kupunguza uzito. 

Zoezi hilo linatarajiwa kuanza mpaka idadi ya washiriki itakapofika 30 ambapo kwa taarifa za awali inaelezwa ni watu 8 tu ndio waliojiandikisha mpaka sasa, alisema Mr Wang, kocha wa mazoezi kwenye gym hiyo.

Ingawa promosheni ya Gym imewavutia wengi hasa kutokana na zawadi ya gari la kifahari huku wakipunguza uzito, wataalam wa afya wameonekana kuwakosoa waandaaji wa jambo hilo wakisema linaweka maisha ya watu hatarini.

“Kupunguza uzito kwa haraka kiasi hicho kunaweza kuweka mkazo kwenye viungo na hata kuhatarisha maisha,” amesema Dkt. Fu Yansong, akiongeza kwamba “kupunguza uzito kisayansi kunapaswa kufanywa hatua kwa hatua ili ubongo, mafuta ya mwili, misuli, na viungo viweze kuzoea usawaziko mpya wa nishati.”

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet