pmbet

Gyökeres agoma kusugua benchi Arsenal, mawakala waanza kumtafutia timu

Eric Buyanza

September 23, 2026
Share :

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden, Viktor Gyökeres, anaripotiwa kutoridhishwa na maisha ndani ya klabu ya Arsenal, huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka kwenye viunga vya Emirates mapema mwezi Januari.

 

Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza kuwa mchezaji huyo amechoshwa na hali ya kusugua benchi, huku kocha Mikel Arteta akionekana kumwamini zaidi Mjerumani Kai Havertz kuongoza safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza.

 

Ripoti zinadodosa kuwa mawakala wa Gyökeres tayari wameanza kuwasiliana na klabu kadhaa kubwa barani Ulaya na Mashariki ya Kati ili kuangalia uwezekano wa usajili wa dharura mwezi Januari.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet