Haijaisha mpaka iishe - Mgunda
Sisti Herman
May 7, 2024
Share :
Baada ya ushindi wa 'Mbinde' wa 2-0 jana dhidi ya Tabora United, kocha Mkuu wa muda wa Simba Juma Mgunda amesema kuwa licha ya utofauti mkubwa wa alama na timu inayoongoza ligi, Yanga, lakini bado hawajakata tamaa kuwania ubingwa wa ligi hadi siku Yanga watakapofikisha alama za kutwangazwa kuwa Mabingwa.
“Tumepata alama 3 na magoli 2 , nawashukuru wachezaji wangu kwa jitihada walizozionesha lakini cha pili nawashukuru wakiokuja kutusapoti”
“Tunajiandaa na mechi nyingine hii tayari imeisha ,sisi tutashindana haiwi mwisho mpaka ifike mechi ya mwisho , sisi tutaendelea kushindana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri mwishoni ndio tuangalie sasa nani ni nani na kipi ni kipi” alisema Mgunda baada ya mchezo.
Simba nafasi ya 3 wakiwa na alama 53 baada ya michezo 24 huku Yanga wakiwa na alama 65 baada ya michezo 25.