pmbet

"Haijalishi unapenda wanawake vipi, epuka sana wake za watu" - Yul Edochie

Eric Buyanza

June 19, 2024
Share :

Muigizaji maarufu wa filamu za Ki-Nigeria ambaye pia ni mchungaji wa Kanisa la True Salvation Ministry, Yul Edochie, amewaonya wanaume wenzake kuacha tabia za kulala na wake za watu.
 

Akiwahubiria waumini wa kanisa lake mtandaoni hivi majuzi, Yul alionya kuwa kulala na mwanamke aliyeolewa humdhoofisha mwanamume kiroho na kumfanya awe rahisi kushambuliwa.
 

“Mwanaume anayelala na wake za watu, ni rahisi sana kwake kupata mashambulizi ya kiroho....Mwanaume hata kama unapenda wanawake kiasi gani, epuka sana wake za watu, epuka kulala na wake za watu. Ni uharibifu. Itakudhoofisha kiroho.” alisema

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet