Haijawahi kunikwaza wasanii kufanya video na Madirector wa nje - Travellah
Eric Buyanza
May 18, 2024
Share :
Muandaaji na muogozaji wa video za muziki @travellah amefunguka na kusema kuwa haijawahi kumkata au kumkwaza kwa wasanii kwenda kurekodi video zao nje ya nchi na waongozaji wengine kwa sababu wasanii hao hufanya vitu kwa 'trend'.
Travellah ameongeza kwa kusema waongozaji wa nje ya nchi huwa wanatoza hela yingi kufanya kazi na wasanii wetu, hivyo hakuna msanii atakayeweza kufanya kazi na 'Madirector' hao kwa muda mrefu, na hivyo wasanii hao huamua kurudi nyumbani.