pmbet

Haikuwa rahisi, mwanariadha huyu aitoa Tanzania kimasomaso

Eric Buyanza

December 4, 2023
Share :

Mwanariadha nyota wa kimataifa wa Tanzania Gabriel Geay ametoa maoni yake baada ya kumaliza nafasi ya tano kwenye mashindano ya Valencia Marathon yaliyofanyika jana jijini Valencia nchini Hispania na kuhudhuriwa na wanariadha nyota waliopo kwenye nafasi za juu kwenye msimamo wa mbio ndefu ulimwenguni.
 

"Haikuwa kazi rahisi leo, nafuraha kwa matokeo nliyopata, nashukuru kwa kila mmoja aliyeniunga mkono, kazi nzuri kwa waandaaji wa Valencia Marathon kwa maandalizi ya tukio hili la kustaajabisha" aliandika hivyo Geay kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Geay alimaliza nafasi ya tano baada ya kukimbia umbali wa kilometa 42 kwa masaa 2:04:33 akiachwa dakika 3 na sekunde 15 tu na Sisay Lemma raia wa Ethiopia aliyekuwa kinara wa mbio hizo.
 

Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa kimataifa wa kukusanya na kuhifadhi takwimu za riadha, World Athletic, Geay yupo nafasi ya 9 kwenye viwango vya riadha vya muda wote akiwa na rekodi ya kukimbia umbali wa kilometa 42 kwa saa 2:03:00, rekodi aliyoweka desemba 4 mwaka 2022, kwenye orodha hiyo yeye ni mtanzania pekee kati ya wanariadha 100 bora wa muda wote ulimwenguni, orodha ikiongozwa na Mkenya Kelvin Kiptum.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet