Hajajibu swali la 7 kwenye mitihani ili amuenzi Ronaldo
Sisti Herman
November 22, 2026
Share :

Kijana mmoja nchini Kenya aliyemaliza kidato cha nne amedai kuwa aliacha kujibu swali la saba katika karatasi zote za mitihani yake ya KCSE, akifanya hivyo kama njia ya kumuenzi nyota wa soka na shujaa wake, Cristiano Ronaldo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kijana huyo alifanya uamuzi huo kutokana na mapenzi yake kwa Ronaldo, ambaye anajulikana kwa kutumia jezi yenye namba saba katika maisha yake ya soka.





