Hakikisha akaunti ya mwanamke wako imeshiba kama yako!
Eric Buyanza
January 4, 2024
Share :
Mwanaume mmoja huko nchini Ghana aitwae Michael Houston, amefichua kuwa wake zake amewapa mamlaka kamili ya kutumia akaunti zake za benki.
Michael, ambaye alifunga ndoa na wanawake hao wiki chache zilizopita, anasema...
"Kwenye uhusiano hakikisha akaunti ya mwanamke wako imeshiba kama yako. Kwa upande wangu wake zangu wote (wawili) wana haki zote za kutumia akaunti zangu za benki muda wowote wanaojisikia, lakini pia na akaunti zao zimeshiba kama zangu, kuwapa uwezo huu kunawafanya wawe na nidhamu ya matumizi...pamoja na uwezo walionao lakini bado wanaomba ruhusa kabla ya kwenda kufanya matumizi yoyote ya ziada ambayo kwa kweli wanastahili na ni jukumu langu," aliandika.