pmbet

Hakimu anaswa kwa kujigeuza mwanamke ili amfanyie mpenzi wake mtihani

Eric Buyanza

May 13, 2026
Share :

Kuna visa vingine kwenye hii dunia ukivisikiliza vinaweza kukupa mshtuko.

 

Huko nchini Uganda mwanaume mmoja aliyewahi kuwa hakimu wa daraja la juu aliyefahamika kwa jina la Ssemwogerere Ammaari Musa alipoteza kibarua chake cha uhakimu na kufunguliwa mashtaka baada ya kunaswa akifanya mtihani wa sheria kwa niaba ya mpenzi wake (Irene Mutonyi) huku akiwa amevaa mavazi ya kike.
 

NINI KILITOKEA

 

Mnamo Ijumaa ya tarehe 28 Julai 2023, Ssemwogerere alikamatwa akiwa darasani akijifanya yeye ndiye Irene Mutonyi akijiandaa kuanza kufanya mtihani.

 

Wakati anakamatwa alikuwa ametengeneza matiti ya bandia, amevaa hereni, amesuka nywele huku akiwa na kitambulisho cha kufoji chenye sura ya kike ili tu kuwahadaa wasimamizi wa mtihani.
 

Tume ya Utumishi wa Mahakama nchini humo ilifuta uteuzi wake mara moja baada ya kashfa hiyo kuibuka.
 

Alikamatwa na kufunguliwa mashtaka rasmi ya kughushi na kujifanya mtu mwingine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet