pmbet

“Hakuna anayeliuza soka” - FIFA

Eric Buyanza

July 31, 2026
Share :

FIFA imesema inaheshimu maoni na wasiwasi uliotolewa hadharani, huku ikisisitiza kuwa itaendelea na mchakato wa mashauriano kwa uwazi na kidemokrasia.

"Tutaendelea na mchakato huu wa mashauriano ili kuhakikisha kila Shirikisho Mwanachama (MA) linapata nafasi ya kupiga kura kwa kuzingatia ukweli na taarifa sahihi."

 

FIFA pia imekanusha vikali madai kuwa kuna mpango wa "kuuza soka".

"Hakuna anayeliuza soka. Hili si jambo ambalo FIFA inaweza kulikubali au kulifikiria kufanya."


Kauli hiyo inakuja wakati mjadala kuhusu mipango mipya ya wadau wa Kombe la Dunia ukiendelea kuzua hisia tofauti katika ulimwengu wa soka.

FIFA inapanga kuanzisha kampuni tanzu ya kibiashara itakayokuwa na jukumu la kusimamia mashindano yake makubwa, ikiwemo Kombe la Dunia.

 

Kupitia kampuni hiyo mpya itakayoitwa FIFA Forward Enterprise (FFE), FIFA itaruhusu wawekezaji kutoka nje kununua hisa za umiliki wa sehemu ya kampuni.

Hata hivyo, FIFA imesisitiza kuwa wawekezaji hao watakuwa na hisa za wachache (minority shares) na hawatakuwa na mamlaka ya kuendesha au kudhibiti kampuni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet