Hakuna haja ya fomu Urais, Samia ndiye mgombea wetu - Wassira
Eric Buyanza
March 28, 2024
Share :
Mwanasiasa mkongwe Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Stephen Wassira, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina sababu ya kuchapa fomu kwa ajili ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, kwani chama hicho tayari kina mgombea (Rais Samia Suluhu Hassan).
Wassira amesema hayo juzi usiku wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Twende Pamoja kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten, jijini Dar es Salaam.
“Nimesikia baadhi ya watu wanasema fomu ni moja kwa mgombea urais wa CCM, mimi nasema fomu hiyo ni ya nini? Katibu Mkuu (Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi) mwenyewe ataamua kama ana hela ya kuchapa fomu hiyo moja, lakini mimi ushauri wangu kwake hakuna haja hata ya fomu hiyo.”