"Hakuna mshambuliaji wa kati anayemzidi Mbappe" - Ancelotti
Sisti Herman
January 20, 2025
Share :
Baada ya jana Kylian Mbappe kufunga magoli mawili yaliyoisaidia Real Madrid kushinda 4-1 dhidi ya Las Palmas kwenye mchezo wa ligi kuu Hispania, kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti baada ya mchezo amewaambia waandishi wa habari kuwa kwasasa hakuna mshambuliaji bora wa kati kumzidi Mbappe.
"Tunaweza kumchezesha pembeni, lakini mimi nakwambia kwasasa hakuna mshambuliaji bora wa kati duniani kumzidi Mbappe"
"Kwangu mimi Mbappe ni mshambuliaji bora kwasasa duniani"
Alinukuliwa Ancelotti mara baada ya mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu.