"Hakuna mtumishi wa Tanesco atakayeruhusiwa kwenda likizo kipindi hiki cha mgao" - Biteko
Eric Buyanza
February 23, 2024
Share :
Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo zote kwa wafanyakazi wote wa Tanesco akiwataka wawepo kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme unaolikabili Taifa hivi sasa.
Biteko amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atakayeruhusiwa kwenda likizo kipindi hiki cha mgawo wa umeme na kwamba, kila mmoja kwenye eneo lake atatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
Dk Biteko ametoa agizo hilo leo Ijumaa, Februari 23, 2024 wakati alipotembelea chanzo cha kuzalisha umeme cha Kidato mkoani Morogoro.