pmbet

"Hakuna mwenye taarifa za Feisal zaidi ya Feisal mwenyewe" - Mkeyenge

Eric Buyanza

July 28, 2025
Share :

Hadithi ya Fei juu ya kuondoka au kubakia Azam FC imeanza kukera. Leo unaamka na kukutana na taarifa inayosema FEI NA YANGA SC KILA KITU SAFI. 

Mtu yule yule ambaye jana alikuandikia taarifa hiyo, leo ameibuka na taarifa nyingine ya FEI AMEMALIZANA NA SIMBA SC. Hujui ushike lipi. Katika muda unaotafakari maandiko hayo unakutana na taarifa nyingine inayosema FEI KUBAKIA AZAM FC. Unazidi kuchanganyikiwa. 

Usajili huu hauna tofauti na ulivyokuwa usajili wa Khalidou Koulibally kujitoa katika makucha ya SS Napoli. Koulibally kabla hajaondoka pale Napoli maandiko ya kuondoka yalikuwa mengi. Alihusishwa na kila timu kubwa. Wasomaji hatukujua tushike lipi. Imetokea hii kwa Feisal. 

Naamini kuna muda Feisal akiwa mwenyewe ameshika simu yake na kutazama yanayoendelea Instagram atakuwa anashangaa na kuangua kicheko. Inachekesha. 

Mpaka sasa hakuna mwenye taarifa sahihi ya Feisal zaidi ya Feisal mwenyewe. Kinachofanyika sasa kwa watoa taarifa za Feisal wengi hatuna majibu ya kuwapa wasomaji wetu. Kinachofanyika sasa ni kutafuta Followers.

Ameandika @abdulmkeyenge1 (Mkunga)

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet