pmbet

Hakuna wa kuongoza nchi iwe, nje au ndani ya CCM zaidi ya Dkt Samia - Sumaye

Eric Buyanza

June 1, 2024
Share :

Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema hakuna mtu yoyote kutoka nje na ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) atakayeweza kuiongoza nchi ya Tanzania zaidi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. 

Sumaye amesema hayo jana Mei 31, 2024 wakati akizungumzia na wananchi wa Katesh Wilaya ya Hanang, katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa ameongozana na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano Kimataifa (Suki), Rabia Abdalla Humid, Ikiwa ni muendelezo wa ziara yao ya kutembelea Mikoa mitano na kukagua utekelezwaji wa Ilani ya CCM.

Sumaye amesema, kutokana na kazi kubwa ya kuendele kuleta maendeleo katika Mkoa wa Manyara, ni vyema wananchi wakaunga kwa pamoja kumuunga mkono Rais huyo kwa kumpa kura nyingi katika chaguzi zijazo ili chama hicho kiendelee kuwepo kwa ajili ya kupata maendeleo zaidi.
TM

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet