"Hakuna wa kutupokonya sisi alama 15" Mzee wa Yanga.
Joyce Shedrack
June 5, 2025
Share :
Wazee wa klabu ya Yanga wameweka wazi msimamo wa timu yao kuhusu mchezo namba 184 kati ya Yanga na Simba huku wakisema hawatacheza na hakuna wa kuwapokonya alama 15.
"Tarehe 15 ndio itatoa taswira ya mechi yetu ya Juni 18, tukipokonywa hizo alama 15 ligi itakuwa imeishia hapo kwanza hakuna Kiongozi wa kutupokonya sisi alama 15 yaani wakijaribu tu ligi itakuwa imeisha."- Shabani Omary (UDA) Mzee wa Yanga SC.
Wazee hao wamewaomba mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kutoshughulika kuja Dar kwa wale wa mkoani kwa ajili ya
mchezo wa derby kwani haupo.
Lakini pia wamevitaka vyombo vya habari kutokutangaza au kufanya promotion kwaajili ya mchezo wa Juni 15 kwa kuitaja Yanga.
Wazee wamewaonya viongozi kutokupeleka timu uwanjani na kama ikitokea wamepeleka basi njia ni nyeupe kwao kuondoka.