pmbet

Halima aongoza kwa kura za 'Tovuti' Miss World

Eric Buyanza

February 23, 2024
Share :

Mlimbwende anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindo ya urembo ya dunia (Miss Wold) yanayofanyika nchini India, Halima Kopwe, amewataarifu watanzania kupitia ukurasa wake wa Insta kwamba kwasasa anaongoza (namba 1) kwenye kura zilizopigwa kupitia website (Tovuti) na hivyo kuwaomba watanzania waendelee kumuunga mkono ili aweze kubaki kileleni.
 

"Hadi sasa, tumeweza kushikilia namba moja kwa kura kwenye upande wa website visits. Ili kuniwezesha kubaki kileleni, tembelea website ya miss world iliopo kwenye bio yangu na kufuatilia matukio yangu mara kwa mara"
 

Haya yanakuwa mashindano ya 71 toka kuanzishwa kwake, fainali za mwaka huu zitafanyika jijini Mumbai nchini India Machi 09, 2024.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet