Halland alivyowekwa mfukoni na Rudigar, Madrid 3-3 City
Sisti Herman
April 10, 2024
Share :
Ikiwa ni wiki moja tu tangu apondwe vikali na kiungo wa zamani wa Manchester United Roy Keane kutokana na kiwango chake uwanjani, mshambuliaji wa Manchester City Erling Halland jana ameendeleza kiwango kibovu baada ya kushindwa kufurukuta mbele ya mabeki wa Real Madrid huku Antonipo Rudigar akimkomalia sana.
Kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya 3-3 kwenye dimba la Santiago Bernabeu Halland aliondoka uwanjani akiwa na takwimui mbaya sana kwani;
- Aligusa mpira mara 20
- Alipiga shuti moja tu
- Hakukokota mpira
- Hakufunga
- Hakutoa pasi ya goli
- Amepoteza mipira 7
- Kati ya pasi 9 alizopiga pasi 3 hazikuwa sahihi
Je unaungana na Roy kusema kuwa Halland ni kama mchezaji wa ligi daraja la pili?