Halland na Lewandowski wakutana Barca ikiitandika Man City
Sisti Herman
July 31, 2024
Share :
Ukiwa ni mwendelezo wa mechi za maandalizi ya msimu mpya kwenye ziara za timu kubwa barani Ulaya zinazoendelea huko nchini Marekani Alfajiri ya leo klabu ya Manchester City ya Uingereza imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Barcelona ya Hispania, Man City wakichapwa kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 2-2 kwenye dakika 90 za mchezo.
Kwenye mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Camping World Stadium jijini Orlando magoli ya Man City yalifungwa na O’Riley dakika 39 na Grealish dakika ya 59 huku ya Barcelona yakifungwa na Victor dakika ya 24 na Torres dakika ya 45+
Mchezo huo pia umewakutanisha washambuliaji wa kati hatari zaidi duniani kwasasa Robert Lewabdowski na Erling Halland ambao walipata wasaa wa kubadilishana jezi.