Hamas yakubali kuwaachia mateka 10 wa Israel
Eric Buyanza
July 10, 2025
Share :
Kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas limesema litawaachia huru mateka 10 wa Israel.
Hatua ya Hamas ni sehemu ya makubaliano ya mazungumzo ya kusitisha mapigano kwa siku 60 huko Gaza baada ya Israel kuonyesha matarajio ya kufikiwa kwa mpango huo.
Mjumbe maalum wa Marekani huko Mashariki ya Kati Steve Witkoff amesema sehemu ya mpango huo itakuwa ni kuwarejesha mateka 10 walio hai.
Hata hivyo Hamas wanaendelea kushinikiza kwamba Israel inatakiwa kuviondoa vikosi vyake vyote huko Gaza.