Hamas yakubali kuweka chini silaha kwa masharti.
Joyce Shedrack
July 31, 2026
Share :
Hamas imesema imekubali kuweka chini silaha baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza kuwa Bodi ya Amani imefikia makubaliano aliyoyataja kuwa ya "kihistoria", kwa mujibu wa afisa mwandamizi wa Hamas aliyelizungumza na BBC.

Kwa mujibu wa pendekezo hilo, mchakato utafanyika kwa awamu ambapo:Hamas itaweka chini silaha.
Vikosi vya Israel vitaanza kujiondoa kadri hatua ya kusalimisha silaha inavyoendelea.
Kikosi cha kimataifa cha ulinzi kitashirikiana na jeshi jipya la polisi wa Palestina kusimamia usalama hadi serikali mpya ya Palestina itakapochukua uongozi wa Gaza.
Donald Trump amezishukuru Misri, Qatar na Uturuki kwa juhudi zao za upatanishi zilizosaidia kufanikisha makubaliano hayo.
Hata hivyo, afisa mwandamizi wa Hamas amesema hatua ya kuweka chini silaha itatekelezwa ikiwa tu Israel itatimiza masharti ya makubaliano, ikiwemo kujiondoa Gaza, kuruhusu kuundwa kwa kamati ya kitaifa ya Palestina na kuanza kwa shughuli za ujenzi upya wa eneo hilo.





