HAMAS/ISRAEL: Rais Biden ana tumaini la kupatikana muafaka kabla ya mwezi wa Ramadhani
Eric Buyanza
March 2, 2024
Share :
Rais wa Marekani Joe Biden amesema anatarajia kupatikana kwa muafaka wa kusitisha vita kati ya wapiganaji wa Hamas na Israeli kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Kauli ya Biden imekuja wakati huu jamii ya kimataifa ikitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru kufuatia hatua ya wanajeshi wa Israeli kutekeleza shambulio katika eneo la kutoa chakula cha msaada kwa raia wa Palestina kaskazini mwa mji wa Gaza.
Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas inasema zaidi ya watu 100 waliuawa katika shambulio hilo.